WCF Yafanikiwa Kuwalipa Wanufaika 10,454 Shilingi bilioni 49.44 toka Kuanzishwa kwake

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umefanikiwa kulipa fidia stahiki ya jumla ya Shilingi bilioni 49.44 kwa wakati kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi takriban wanufaika 10,454 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2015.  Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma